{"id":82,"date":"2020-05-14T08:57:59","date_gmt":"2020-05-14T08:57:59","guid":{"rendered":"https:\/\/www.ubungoanglican.or.tz\/?page_id=82"},"modified":"2026-09-23T14:07:44","modified_gmt":"2026-09-23T14:07:44","slug":"historia","status":"publish","type":"page","link":"https:\/\/www.ubungoanglican.or.tz\/en\/kuhusu-kanisa\/historia\/","title":{"rendered":"History"},"content":{"rendered":"<h1 class=\"wp-block-heading\">Historia ya Parish ya Mt. Batholomayo \u2013 Ubungo<\/h1>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Maadhimisho ya Jubilei ya Dhahabu ya mwaka 2026 yanaadhimisha miaka 50 tangu mwaka 1976, mwaka ambao ujenzi wa Kanisa la kwanza ulianza rasmi na Kanisa likapewa jina la Mtakatifu Batholomayo na Askofu John Sepeku. Hata hivyo, mizizi ya huduma ya Ubungo inaanzia mwaka 1971. Hivyo historia ya Jubilei hii ni safari ya zaidi ya nusu karne ya imani, uinjilisti, kujitoa na maendeleo.<\/p>\n\n\n\n<h2 class=\"wp-block-heading\"><a>Mwanzo wa huduma chini ya mti wa mwembe<\/a><\/h2>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Historia ya Mt. Batholomayo \u2013 Ubungo inaanzia mwaka 1971, wakati waumini wachache wa eneo la Ubungo walipoanza kukutana kwa ibada kwa kujiongoza wenyewe chini ya mti wa mwembe uliokuwa pembezoni mwa majengo ya Shule ya Msingi NHC. Miongoni mwa waumini wa mwanzo waliokuwa na maono ya kuanzisha huduma hiyo alikuwa Bwana Arthur Pauseki. Mwaka 1972, kundi hilo lilipata ruhusa ya kutumia darasa katika Shule ya Msingi NHC kwa ibada na shughuli za kiroho. Kumbukumbu inawataja pia Mary Kilowaka Mapunda, Mzee Martin Mvaa, Mzee Daniel Yona na Veronica Mpombo miongoni mwa waumini wa kipindi hicho.<\/p>\n\n\n\n<h2 class=\"wp-block-heading\"><a>Kuanzishwa kwa Kigango cha Ubungo<\/a><\/h2>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Mwishoni mwa Desemba 1972, waumini walimwona Canon Nathan Kipalamoto wa Kanisa Anglikana Kristo Mfalme Kinondoni na kumweleza kuhusu kundi lililokuwa likikusanyika Ubungo. Taarifa hiyo ilifikishwa kwa Askofu John Sepeku. Mwaka 1973, Ubungo ilianzishwa kuwa Kigango chini ya Kanisa Anglikana Kristo Mfalme Kinondoni. Canon Nathan Kipalamoto na Mapadre wengine waliendelea kutoa huduma za kiroho hadi mwaka 1975.<\/p>\n\n\n\n<h2 class=\"wp-block-heading\"><a>Uongozi wa kiroho na kupatikana kwa kiwanja<\/a><\/h2>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Mwaka 1975, Robinson Crispo Komba aliteuliwa kuwa Mwinjilisti wa kwanza wa Ubungo. Katika mwaka huo huo, Kanisa lilipata kiwanja karibu na Shule ya Msingi NHC \u2013 eneo ambalo Mtaa wa Mt. Batholomayo ulipo sasa \u2013 ili kuondoka katika mazingira ya kuabudia darasani na kuwa na eneo maalumu la Kanisa.<\/p>\n\n\n\n<h2 class=\"wp-block-heading\"><a>Ujenzi wa Kanisa la kwanza na jina la Mt. Batholomayo<\/a><\/h2>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Mwaka 1976 ulikuwa hatua ya msingi katika historia ya Mtaa. Ujenzi wa jengo la kwanza la Kanisa ulianza rasmi, na Askofu John Sepeku akalipa Kanisa jina la Mtakatifu Batholomayo. Katika kipindi hicho pia ilijengwa nyumba ya kwanza ya watumishi. Awamu ya kwanza ya ujenzi ilikamilika mwaka 1978 na kuzinduliwa rasmi na Askofu John Sepeku. Hii ndiyo sababu mwaka 2026 unaadhimishwa kama Jubilei ya miaka 50 tangu kupewa jina la Mt. Batholomayo na kuanza kwa ujenzi rasmi wa Kanisa.<\/p>\n\n\n\n<h2 class=\"wp-block-heading\"><a>Upanuzi wa Kanisa na huduma za kijamii<\/a><\/h2>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Kutokana na ongezeko la waumini, mwaka 1981 iliamuliwa kupanua jengo la Kanisa la awali chini ya uongozi wa Canon Nathan Kipalamoto. Sambamba na huduma za kiroho, Mtaa ulihusika pia katika huduma za kijamii. Tangu mwaka 1980 kulikuwapo Zahanati ya Dayosisi katika eneo la Mtaa, iliyohudumia wakazi wa Ubungo na maeneo ya jirani. Zahanati hiyo ilibomolewa Aprili 2009, kwa kibali cha Askofu wa Dayosisi, ili kupisha ujenzi wa Kanisa jipya.<\/p>\n\n\n\n<h2 class=\"wp-block-heading\"><a>Ujenzi wa Kanisa jipya la kisasa<\/a><\/h2>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Wazo la kujenga Kanisa jipya lilianza mwaka 2005 chini ya uongozi wa Canon Julius Kiondo, kutokana na ongezeko la waumini kiasi kwamba baadhi yao walilazimika kukaa nje wakati wa ibada za Jumapili. Ujenzi ulianza Aprili 2009 chini ya uongozi wa Rev. Amani Chitemo. Jengo hilo kubwa la kuabudia limekuwa mojawapo ya hatua muhimu za maendeleo ya Mtaa.<\/p>\n\n\n\n<h1 class=\"wp-block-heading\"><a>Safari ya Miaka 50: 1976\u20132026<\/a><\/h1>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-table\"><table class=\"has-fixed-layout\"><thead><tr><td><strong>Mwaka\/Kipindi<\/strong><\/td><td><strong>Kumbukumbu Kuu<\/strong><\/td><\/tr><\/thead><tbody><tr><td>1971<\/td><td>Waumini wachache waanza ibada chini ya mti wa mwembe karibu na Shule ya Msingi NHC.<\/td><\/tr><tr><td>1972<\/td><td>Waumini wapata darasa la Shule ya Msingi NHC kwa ibada; mwishoni mwa mwaka wawasiliana na Canon Nathan Kipalamoto.<\/td><\/tr><tr><td>1973<\/td><td>Ubungo yaanzishwa kuwa Kigango chini ya Kristo Mfalme Kinondoni kwa uamuzi wa Askofu John Sepeku.<\/td><\/tr><tr><td>1975<\/td><td>Robinson Crispo Komba awa Mwinjilisti wa kwanza; Kanisa lapata kiwanja chake.<\/td><\/tr><tr><td>1976<\/td><td>Ujenzi wa Kanisa la kwanza waanza; Kanisa lapewa jina la Mtakatifu Batholomayo; nyumba ya watumishi yajengwa.<\/td><\/tr><tr><td>1978<\/td><td>Awamu ya kwanza ya ujenzi yakamilika na kuzinduliwa na Askofu John Sepeku.<\/td><\/tr><tr><td>1980<\/td><td>Zahanati ya Dayosisi katika eneo la Mtaa yatoa huduma kwa jamii.<\/td><\/tr><tr><td>1981<\/td><td>Jengo la Kanisa la awali lapanuliwa kutokana na ongezeko la waumini.<\/td><\/tr><tr><td>2005<\/td><td>Wazo la kujenga Kanisa jipya la kisasa laanza chini ya Canon Julius Kiondo.<\/td><\/tr><tr><td>Aprili 2009<\/td><td>Ujenzi wa Kanisa jipya waanza chini ya Rev. Amani Chitemo; zahanati yabomolewa kupisha ujenzi.<\/td><\/tr><tr><td>2026<\/td><td>Mt. Batholomayo \u2013 Ubungo yaadhimisha Jubilei ya Dhahabu ya miaka 50 (1976\u20132026).<\/td><\/tr><\/tbody><\/table><\/figure>\n\n\n\n<h1 class=\"wp-block-heading\">Kamati na Idara za Mtaa<\/h1>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Katika safari yake ya huduma, Mtaa wa Mt. Batholomayo \u2013 Ubungo umeendelea kujenga mfumo wa uongozi na ushirikishwaji wa waumini kupitia Kamati na Idara mbalimbali. Vyombo hivi vinasaidia kuratibu maeneo ya kiroho, kiutawala, kifedha, maendeleo, malezi, afya, mazingira na huduma kwa makundi mbalimbali ya waumini.<\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-table\"><table class=\"has-fixed-layout\"><thead><tr><td><strong>Na.<\/strong><\/td><td><strong>Kamati\/Idara<\/strong><\/td><\/tr><\/thead><tbody><tr><td>1<\/td><td>Kamati ya Utendaji<\/td><\/tr><tr><td>2<\/td><td>Kamati ya Fedha<\/td><\/tr><tr><td>3<\/td><td>Kamati ya Mipango, Uchumi na Maendeleo<\/td><\/tr><tr><td>4<\/td><td>Kamati ya Ujenzi na Miundombinu<\/td><\/tr><tr><td>5<\/td><td>Kamati ya Ndoa na Malezi<\/td><\/tr><tr><td>6<\/td><td>Kamati ya Uinjilisti<\/td><\/tr><tr><td>7<\/td><td>Kamati ya Afya na Mazingira<\/td><\/tr><tr><td>8<\/td><td>Kamati ya Ibada na Itifaki<\/td><\/tr><tr><td>9<\/td><td>Idara ya Watoto, Makuzi na Elimu ya Dini Mashuleni<\/td><\/tr><tr><td>10<\/td><td>TAYO<\/td><\/tr><tr><td>11<\/td><td>UBAKI<\/td><\/tr><tr><td>12<\/td><td>UMAKI<\/td><\/tr><\/tbody><\/table><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Ushirikiano wa Kamati na Idara hizi unaonesha kwamba huduma ya Mtaa inatekelezwa kwa pamoja, kila mmoja akitumia nafasi na karama zake katika kulijenga Kanisa. Kama inavyofundisha 1 Wakorintho 12:5\u20136, zipo huduma mbalimbali, lakini Bwana ni yeye yule anayefanya kazi ndani ya wote.<\/p>\n\n\n\n<h1 class=\"wp-block-heading\"><a>Uinjilisti, Ibada na Malezi ya Kiroho<\/a><\/h1>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Jubilei ya Dhahabu inatukumbusha kuwa kusudi la Kanisa halikomi katika kukumbuka historia yake, bali historia hiyo iwe msingi wa kuendeleza utume wa Kristo. Yesu aliwaagiza wanafunzi wake: \u201cEnendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi\u201d (Mathayo 28:19). Hivyo, miaka 50 ya Mtaa wa Mt. Batholomayo \u2013 Ubungo ni wakati wa kumshukuru Mungu na kufanya upya dhamira ya uinjilisti, ibada na malezi ya kiroho.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Katika kutekeleza wajibu huu, Mtaa umeendelea kushiriki katika kuieneza Injili nje ya mipaka yake, ikiwemo kushiriki katika kufungua na kuutunza Mtaa wa Msata uliopo Bagamoyo. Maandalizi ya Jubilei yamejumuisha mafundisho kuhusu shukrani na utume, kwa lengo la kuwaimarisha waamini katika imani na maisha ya ushuhuda.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Mtaa uendelee kujengwa katika Neno la Mungu, maombi, ibada na ushirika. Kanisa la kwanza lilidumu katika mafundisho, ushirika, kuumega mkate na kusali (Matendo 2:42). Malezi ya watoto, vijana na familia yaendelee kupewa kipaumbele ili imani na utume vikabidhiwe kutoka kizazi kimoja kwenda kingine. Kwa hiyo, Jubilei hii iwe mwanzo mpya wa uamsho na utume, kwa kuimarisha maombi, Neno la Mungu, uinjilisti na ushuhuda wa Kikristo katika jamii.<\/p>\n\n\n\n<h1 class=\"wp-block-heading\"><a>Kwaya, Watoto, Vijana na Huduma za Ushirika<\/a><\/h1>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Muziki, uimbaji, kusifu na kuabudu ni sehemu muhimu ya maisha ya kiroho katika Mtaa wa Mt. Batholomayo \u2013 Ubungo. Huduma hizi ni njia ya kumwabudu Mungu, kutoa shukrani, kujenga imani na kueneza Injili. Biblia inatuhimiza: \u201cMwimbieni Bwana wimbo mpya; mwimbieni Bwana, nchi yote\u201d (Zaburi 96:1), huku Wakolosai 3:16 ikiwahimiza waamini kufundishana kwa zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Katika Jubilei ya Dhahabu, huduma za muziki za ndani ya Kanisa zinajumuisha Kwaya Kuu, Kwaya ya Kanaani, Sauti ya Batholomayo, Kwaya ya Itifaki, Kwaya ya Watoto, Kwaya ya UMAKI na Kikundi cha Kusifu na Kuabudu. Wageni wa huduma ya muziki ni AICT Vijana Chang&#8217;ombe Kwaya, Moravian Efatha Choir na Kikundi cha Matarumbeta.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Ushiriki wa watoto na vijana una umuhimu wa pekee, kwa kuwa wao ni warithi na waendelezaji wa imani na utume wa Kanisa. \u201cKizazi kwa kizazi kitayasifu matendo yako\u201d (Zaburi 145:4). Hivyo, Mtaa una wajibu wa kuendelea kuwalea katika Neno la Mungu, maombi, ibada na huduma. Jubilei inakuwa daraja linalounganisha waliotangulia, wanaohudumu sasa na kizazi kitakachoendeleza huduma.<\/p>\n\n\n\n<h1 class=\"wp-block-heading\"><a>Maendeleo ya Mtaa katika Miaka ya Huduma<\/a><\/h1>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Safari ya miaka 50 imeambatana na ukuaji wa kiroho, ongezeko la waumini, maendeleo ya miundombinu, uwekezaji na matumizi ya teknolojia katika huduma. Mambo yafuatayo ni miongoni mwa hatua muhimu zilizofikiwa:<\/p>\n\n\n\n<h2 class=\"wp-block-heading\"><a>1. Ukuaji wa Waumini<\/a><\/h2>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Katika kipindi hiki, idadi ya waumini imeongezeka na kufikia takribani 800. Ukuaji huu unaonesha kupanuka kwa jumuiya ya waamini na pia umeongeza wajibu wa Mtaa katika malezi ya kiroho, uinjilisti, ibada na huduma.<\/p>\n\n\n\n<h2 class=\"wp-block-heading\"><a>2. Ujenzi wa Jengo Kubwa la Kuabudia<\/a><\/h2>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Miongoni mwa hatua kubwa za maendeleo ni ujenzi wa jengo kubwa la Kanisa kwa ajili ya ibada. Jengo hili limeongeza uwezo wa Mtaa kuhudumia waumini wanaoongezeka na kutoa mazingira yanayofaa kwa ibada na shughuli mbalimbali za kiroho.<\/p>\n\n\n\n<h2 class=\"wp-block-heading\"><a>3. Makazi ya Kasisi Kiongozi<\/a><\/h2>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Mtaa umefanikiwa kujenga nyumba ya kisasa kwa ajili ya makazi ya Kasisi Kiongozi, hatua inayoweka mazingira bora ya huduma na kuimarisha miundombinu ya Mtaa.<\/p>\n\n\n\n<h2 class=\"wp-block-heading\"><a>4. Ukumbi wa Mt. Batholomayo<\/a><\/h2>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Jengo lililokuwa Kanisa la zamani limebadilishwa matumizi na kuwa Ukumbi wa Mt. Batholomayo. Kwa namna hii, sehemu muhimu ya historia ya Mtaa imeendelea kutumika katika mikutano, mafunzo, ushirika na shughuli nyingine za Kanisa.<\/p>\n\n\n\n<h2 class=\"wp-block-heading\"><a>5. Majengo ya Kitega Uchumi<\/a><\/h2>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Umoja wa Mama wa Kikristo (UMAKI) umefanikiwa kujenga jengo lake la kitega uchumi. Kwaya Kuu nayo imefanikiwa kujenga jengo la kitega uchumi. Hatua hizi zinaimarisha uwezo wa vikundi na Mtaa kuchangia katika huduma na kujitegemea.<\/p>\n\n\n\n<h2 class=\"wp-block-heading\"><a>6. Uinjilisti na Mtaa wa Msata<\/a><\/h2>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Mtaa wa Mt. Batholomayo umeendelea kutekeleza wajibu wa kueneza Injili na umehusika katika kufungua na kuutunza Mtaa wa Msata uliopo Bagamoyo. Hii ni sehemu muhimu ya matunda ya uinjilisti katika safari ya miaka 50.<\/p>\n\n\n\n<h2 class=\"wp-block-heading\"><a>7. Mawasiliano na Uinjilisti wa Kidijitali<\/a><\/h2>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Mtaa umeanzisha vyombo vya mawasiliano ya kidijitali vinavyosaidia kutoa taarifa, kuhifadhi kumbukumbu na kueneza Habari Njema. Vyombo hivyo vinajumuisha tovuti ya Mtaa, Ubungo Anglican Online TV na majukwaa ya mitandao ya kijamii kama Facebook na Instagram, pamoja na njia nyingine za mawasiliano.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><\/p>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Historia ya Parish ya Mt. Batholomayo \u2013 Ubungo Maadhimisho ya Jubilei ya Dhahabu ya mwaka 2026 yanaadhimisha miaka 50 tangu mwaka 1976, mwaka ambao ujenzi wa Kanisa la kwanza ulianza rasmi na Kanisa likapewa jina la Mtakatifu Batholomayo na Askofu John Sepeku. Hata hivyo, mizizi ya huduma ya Ubungo inaanzia mwaka 1971. Hivyo historia ya &#8230; <span class=\"more\"><a class=\"more-link\" href=\"https:\/\/www.ubungoanglican.or.tz\/en\/kuhusu-kanisa\/historia\/\">[Read more&#8230;]<\/a><\/span><\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":0,"parent":19,"menu_order":0,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","template":"","meta":{"footnotes":""},"class_list":["entry","page","publish","author-","post-82"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/www.ubungoanglican.or.tz\/en\/wp-json\/wp\/v2\/pages\/82","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/www.ubungoanglican.or.tz\/en\/wp-json\/wp\/v2\/pages"}],"about":[{"href":"https:\/\/www.ubungoanglican.or.tz\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/page"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/www.ubungoanglican.or.tz\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/www.ubungoanglican.or.tz\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=82"}],"version-history":[{"count":4,"href":"https:\/\/www.ubungoanglican.or.tz\/en\/wp-json\/wp\/v2\/pages\/82\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":727,"href":"https:\/\/www.ubungoanglican.or.tz\/en\/wp-json\/wp\/v2\/pages\/82\/revisions\/727"}],"up":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/www.ubungoanglican.or.tz\/en\/wp-json\/wp\/v2\/pages\/19"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/www.ubungoanglican.or.tz\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=82"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}